Jumamosi 26 Septemba 2026 - 17:28
Vikosi vya Jeshi la Iran vinazidi kuwa na nguvu siku baada ya siku/ Dkt. Pezeshkian aliifikisha mantiki ya Iran duniani katika Umoja wa Mataifa

Hawza/ Imam wa muda wa Ijumaa wa Tehran amesema: Rais katika hotuba hiyo aliifikisha mantiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran duniank na akaeleza kwa uwazi misimamo ya taifa la Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami, katika Swala ya Ijumaa ya wiki hii ya Tehran iliyofanyika Ijumaa tarehe 3 Mehr H.S, katika Chuo Kikuu cha Tehran, huku akizungumzia umuhimu wa waumini kudumisha utayari wa kuwepo katika uwanja wa mapambano, alisema: Moja ya maswali muhimu ni kwamba Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) aliwezaje kuendelea kuwaweka tayari waumini katika miaka yote ya mapambano na vita; suala ambalo hata leo tunalihitaji.

Aliongeza: Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) alichukua hatua tano za msingi kwa ajili ya jambo hili; kwanza, kujenga na kuimarisha utamaduni wa jihadi; pili, kuimarisha misingi ya kiitikadi; tatu, kujenga matumaini miongoni mwa wanajeshi; nne, kuingiza hofu katika nyoyo za maadui; na tano, kukabiliana kwa uthabiti na vita vya kisaikolojia vya adui.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran aliendelea kusema: Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) aliuweka utamaduni wa jihadi kuwa sehemu ya msingi katika jamii; kama ambavyo leo kuomboleza kwa ajili ya Sayyid al-Shuhadaa (a.s.) umekuwa utamaduni wa jumla katika jamii.

Ayatullah Khatami, akisisitiza nafasi ya vyombo vya habari katika kuimarisha roho ya muqawama, alisema: Vyombo vya habari vya kuona na kusikia vinapaswa kufahamu kwamba uti wa mgongo wa muqawama ni kuimarisha moyo na kujenga matumaini, na suala hili linapaswa kupewa kipaumbele katika shughuli za vyombo vya habari.

Aidha, akizungumzia nafasi ya neema za Mwenyezi Mungu na kuandamana waumini katika ushindi wa mwanzo wa Uislamu, alibainisha: Katika vita vilivyopita, neema za Mwenyezi Mungu na kuandamana waumini ndizo zilizokuwa na nafasi ya kwanza, na vipengele hivi viwili kwa pamoja vilikuwa sababu ya kudumisha utayari wa jamii wa kuwepo katika uwanja wa mapambano.

Imam wa muda wa Ijumaa wa Tehran, huku akisisitiza kwamba kinachomfanya adui awe na hofu ni kuimarika vikosi vya jeshi, aliongeza: Kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, vikosi vyetu vya jeshi vinazidi kuwa na nguvu siku baada ya siku.

Aliongeza: Wananchi wanapaswa kufahamu kwamba hata katika kipindi cha kusitisha mapigano, mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hautapuuza hata kwa muda mfupi utengenezaji wa makombora na kuimarisha uwezo wake wa makombora.

Aliendelea kwa kurejelea kufanyika hafla ya kumuenzi Bibi Ma’suma (s.a.) huko Qum, akasema: Katika wiki iliyopita, hafla ya kumuenzi Bibi Ma’suma (s.a.) ilifanyika Qum, na ilikuwa hafla nzuri.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran pia, akizungumzia kufariki Ayatullah Shubayri Zanjani, alisema: Jumatatu iliyopita ilikuwa siku ya kufariki mwanazuoni mkubwa Ayatullah Shubayri Zanjani; kwa hakika, alikuwa mwanazuoni mkubwa, aliyeishi karibu karne moja, na alikuwa miongoni mwa nguzo imara za Hawza, na katika elimu ya Rijal pia alikuwa na nafasi ya kwanza.

Aliongeza: Kupotea shakhsia hii mashuhuri kumeacha pengo na dosari miongoni mwa watafiti wakuu wa Kishia.

Imam wa muda wa Ijumaa wa Tehran, akiendelea kuzungumzia hotuba ya Rais katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alisema: Kwa hakika, hotuba ya Rais katika Umoja wa Mataifa ilikuwa hotuba yenye mantiki, ya kishujaa na yenye ujasiri; kiasi kwamba aliugeuza Umoja wa Mataifa kuwa mahakama.

Aliongeza: Hotuba hii kwa hakika ilikuwa tafsiri ya kaulimbiu za wananchi za “Mauti kwa Marekani” na “Mauti kwa Israel”, na ilikuwa inastahili taifa ambalo kwa muda wa miezi saba halijaondoka mitaani na ambalo halitaondoka mitaani hadi pale adui atakaposhindwa kabisa.

Ayatullah Khatami alisisitiza: Rais katika hotuba hiyo aliifikisha mantiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran duniank na akaeleza kwa uwazi misimamo ya taifa la Iran.

Aliendelea kusema: Mashirika ya habari ya dunia pia yalizingatia sehemu hii ya hotuba ya Rais na kuweka vichwa vya habari kwamba Iran haitasalimu amri kwa nguvu.

Imam wa muda wa Ijumaa wa Tehran alisema: Rais wa Iran, alimjibu Rais wa Marekani kwa jibu kali na lenye nguvu. Trump hajalifahamu taifa lake mwenyewe na ameiletea Marekani madhara kiasi kwamba amepoteza umaarufu wake; katika historia ya marais wa Marekani, kiwango kama hiki cha kutopendwa hakijawahi kutokea.

Aliongeza: Trump pia hajalifahamu taifa la Iran, na licha ya kushindwa huku mara kwa mara, bado hajafikia ufahamu kwamba taifa la Iran ni taifa la Kiashura na halikubali udhalili wala kusalimu amri.

Ayatullah Khatami, huku akisema kwamba “Haiwezekani sisi tukubali udhalili” kumechanganyika na uwepo wa taifa la Iran, aliendelea: Imam Khomeini (ra) na Imam Shahidi walisisitiza juu ya umoja, na sasa Kiongozi wa Mapinduzi pia anaendelea kusisitiza juu ya umoja, kwa sababu umoja ni jambo la lazima.

Alisema: Umoja unahitaji mhimili, na mhimili wake ni Waliyy al-Faqih; kufuata Wilaya ndilo jambo la msingi, si kutoa kauli za ufuasi wa Wilaya. Mapigo ya kazi yanapaswa kuwa mikononi mwa watu wanaokubali watu hawa na ambao wako tayari kujitoa muhanga kwa ajili yao.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran alisisitiza: Watu walioathiriwa na Magharibi hawawezi kuwa mhimili wa umoja, hawana uhusiano wa aina moja na watu hawa, na hawapaswi kukabidhiwa nyadhifa muhimu.

Aliendelea kuzungumzia suala la hijabu, akasema: Hijabu ni miongoni mwa mambo matakatifu ya taifa hili, na wale wanaotaka umoja katika jamii udumishwe hawapaswi kuchukua hatua katika njia ya kutovaa hijabu. Msizungumze kwa namna ambayo itafanya ionekane kwamba mfumo unaunga mkono watu wasiovaa hijabu; mfumo hauungi mkono kutovaa hijabu.

Ayatullah Khatami aliongeza: Wale ambao hawazingatii hijabu nao ni raia wa taifa hili, na uwepo wao katika mikusanyiko na kuandamana pamoja na wananchi ni jambo zuri, lakini kubeza hijabu na kupinga mambo ya wazi ya dini ni kinyume na umoja.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran, katika sehemu nyingine ya hotuba yake, huku akizungumzia kuanza mwaka wa masomo, alisema: Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi kwa ajili ya kuanza mwaka wa masomo ulikuwa ujumbe muhimu sana, na kwa bahati nzuri nilisikia katika habari kwamba baadhi ya viongozi wanafuatilia kuutekeleza ujumbe huo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha